Afisa wa UM apewa tuzo kwa kusaidia watu wenye ulemavu
Afisa wa Umoja wa Mataifa wametunukiwa hadhi ya heshima nchini Ujerumani kutoakana na kutambuliwa kwa mchango wao uliosaidia kuwajali na kuwapa fursa watu walioko pembezoni hasa makundi ya watu wenye ulemavu.
Mshauri wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya michezo na maendeleo Wilfried Lemke,ametunikiwa nishani ijulikanayo Bobby Mjini Berlin. Tuzo hiyo ambayo inajikita kwenye masuala ya habari imebeba jina la mwanamichezo wa kwanza nchini humo aliyetoa msukumo mkubwa kuwawezesha watu wasiojiweza.
Akizungumzia tuzo hiyo Bwana Lemke ameseam hiyo ni heshima kubwa kwake na kwa Umoja wa Mataifa na kuongeza kuwa siku zote michezo ndiyo njia bora inayoweza kuwafikia makundi ya jamii ya watu wote.
Wakati wa michezo ya walemavu kwa majira ya kiangazi ya mwaka 2008 iliyofanyika kwenye mataifa mbalimbali, Bwana Lemke daima alitumia fursa hiyo kuzungumzia umuhimu wa kuwatambua na kuwajali watu wenye ulemavu.