Skip to main content

Mkutano wa UNESCO kuhusu kulinda utamaduni waanza Nairobi

Mkutano wa UNESCO kuhusu kulinda utamaduni waanza Nairobi

Mkutano wa tano wa kamati za serikali zinazohusika na utunzi wa tamaduni za kale uliondaliwa na shirika la Umoja wa mataifa la elimu , sayansi na utamuduni UNESCO umeng\'oa nanga hii leo hapa mjini Nairobi.

Mkutano huo wa siku tano ambao ndio wa kwanza kuandaliwa barani Afrika umewaleta pamoja zaidi ya wanachama 130 waliofikia makubaliono ya kulinda tamaduni za kale. Akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutaano huo mkurugenzi wa shirika la UNESCO Irina Bokova amesema kuwa makubaliano hayo yanatoa mweleko ya kugundua tamaduni zaidi duniani na pia yana umuhimu katika kutimizwa kwa malengo ya milenia.

Insert..Irina Bokova

"Pia ni njia ya kutambua na kulinda tamaduni zilizo na umuhimu katika kutimizwa kwa malengo ya milenia. Katika kulinda mazingira , kuwainua wanawake , kuboresha afya , kubuni shughuli zinazoleta mapato na kuchangia kuwepo kwa anani na utatuzi wa mizozo. Ninaamini kuwa utamaduni wa kale una umuhimu ambao tunastahili kulinda"

Mkutano huu pia utajadili tamaduni kutoka nchi mbali mbali hususan nchini Croatia na china zilizo kwenye hatari ya kutoweka na ambazo zinaweza kupata ufadhili kutoka kwa shirika la UNESCO. Pia mkutano huo utakagua tamaduni 47 kutoka mataifa 29 na kuamua iwapo ni zipi zinaweza kujumuishwa kwenye orodha ya tamaduni za kale na iwapo zimekuwa zikilindwa na kutumiwa na jamii husika.