Wakati dunia ikiadhimisha siku ya kisukari, Ban asisitiza haja ya kutambua na mapema dalili za ugonjwa huo

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya kisukari, Ban asisitiza haja ya kutambua na mapema dalili za ugonjwa huo

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya kisukari duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amehimiza haja ya kuwepo kwa hatua za awali za kutambua dalili za ugonjwa huo na kufuatiwa na matibabu ya uhakika ili kuepusha vifo visivyo vyalazima vinavyotokana na ugonjwa huo.

Amesisitiza kuwa suala la kugundua mapena dalili za ugonjwa huo ni hatua muhimu na inayohitaji kuzingatiwa na kila mmoja kwani kwa kufanya hivyo wengi wanaweza kuokoa maisha yao.

Kwa mujibu wa takwimi zilizotolewa na shirika la afya ulimwenguni WHO, vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huu wa kisukari vinaweza kuongezeka mara mbili hadi kufikia 2030 kwa mwaka, huku nchi maskini zikitajwa kuwa katika hatari zaidi.

Kwa hivi sasa ugonjwa wa kisukari umekuwa ukiwakumba zaidi ya watu milioni 220 na hakuna nchi inayoweza kusema kwamba ipo salama