Skip to main content

Hatua zinahitajika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa: UM

Hatua zinahitajika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa: UM

Afisa wa Umoja wa Mataifa anayehusika na mabadiliko ya hali ya hewa amasema kuwa hatua zaidi zinastahili kuchukuliwa katika nyanja za kitaaifa na kimataifa ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Akiongea mjini Bonn nchini Ujerumani kabla ya mkutano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ambao utaandaliwa mjini Cancun nchini Mexico bibi Christiana Figueres amesema kuwa tayari nchi kadha zimechukua hatua zikiwemo kuweka sheria ili kuzua mabadiliko ya hali ya hewa na kuongeza kuwa ni lazima kubaini kile kinachofanyika kwenye ngazi za kitaifa na kiamataifa.

(SAUTI CHRISTIANA FIGUERES)