Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hasara za majanga asili huenda zikaongezeka mara tatu: Bank ya dunia

Hasara za majanga asili huenda zikaongezeka mara tatu: Bank ya dunia

Ripoti mpya ya pamoja ya Bank ya dunia na Umoja wa Mataifa inasema hasara za kila mwaka zitokanazo na majanga ya asili huenda zikawa mara tatu ifikapo mwisho wa karne hii hata bila kujumuisha athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kuongeza maafa ya dola bilioni 22 hadi 68 kila mwaka kutokana na vimbunga pekeee. Ripoti hiyo pia imesema idadi ya watu walio katika hatari ya kukumbwa na vimbunga na matetemeko ya ardhi mijini inaweza kuongezeka mara mbili na kufikia bilioni 1.5 ifikapo 2050.

Ripoti hiyo iliyopewa kichwa "majanga ya asili, majanga yasiyo ya asili na njia za kiuchumi za kuyazuia" imetolewa leo miji Washington. Ikiwalenga mawaziri wa fedha ripoti hiyo inasisitiza kwamba kukinga kunafaida lakini sio lazima kila wakati utumie gharama kubwa kuzuia. Inataja njia kadhaa za kuzuaia vifo na uharibifu utokanao na majanga ya asili kama matetemeko ya ardhi, vimbunga na mafuriko.

Ni njia nyepesi na za kutumia mtazamo wa ufahamu kwa mfano serikali zinaweza kuwezesha kupatikana kwakirahisi taarifa za athari na hatari iliyoko, pia kutoka hati za kumiliki ardhi kunaweza kusaidia uwezekano wa kuondolewa kwa nguvu au kubomolewa nyumba zao, na kuwachagiza watu kuwekeza katika ujenzi na miundombinu salama na kuchukua hatua hizi hakutozigharimu serikali fedha nyingi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo katika kipindi cha miaka 40 hadi kufikia 2010 majanga ya asili yamekatili maisha ya watu milioni 3.3 na milioni moja wamekufa barani Afrika kutokana na ukame pekee.