Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO lazishauri mataifa ya G20 kungazia suala la ajira

ILO lazishauri mataifa ya G20 kungazia suala la ajira

Shirika la kazi duniani ILO limezatika nchi tajiri duniani na zile zinazoinukia kiuchumi za G20 kuangazia zaidi suala la ajira na sera zinazochangia kuongezeka kwa nafasi za kazi kwenye mkutano wa nchi hizo unaotarajiwa kuandalia mjini Seoul nchini Korea Kusini.

Hata kama kumeshuhudia ongezeko la nafasi za ajira kwenye nchi hizi zote mwaka huu hususan zile zinazoinukia kiuchumi bado ripoti hiyo inaonyesha kuwa nafasi hizo za ajira hazijakuwa na uwezo wa za kupunguza idadi ya waliokosa ajira wakati wa hali mbaya ya kiuchumi iliyoikumba dunia. ILO linasema kuwa mataifa ya G20 yatahitaji kubuni nafasi za ajira milioni 21 kila mwaka.