Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushindani ulio wa haki utachangia wa maendeleo duniani

Ushindani ulio wa haki utachangia wa maendeleo duniani

Maafisa wa ngazi za juu serikalini na wakuu wa mashirika ya ushindani wa kibiashara wametoa wito wa kuwepo kwa ushindani ulio wa haki wa kiuchumi wakati nchi zinapojikakamua kujikwamua kutokana na hali mbaya kichumi.

Mkutano huo wa juma moja utaangazia sheria za Umoja wa Mataifa kuhusu biashara. Wazungumzaji waliofuata walisema kuwa sera za serikali bila kujali hali ya uchumi wa nchi zitahitaji kulenga zaidi ushindani wa kibiashara badala ya kukandamiza ushindani huo.