Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa uhamiaji na maendeleo wang'oa nanga Mexico

Mkutano wa uhamiaji na maendeleo wang'oa nanga Mexico

Mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu Navi Pillay aliye pia mwenyeki wa sasa wa mashirika 16 ya uhamiaji duniani anamwakilisha katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwenye mkutano muhimu uliong\'oa nanga leo mjini Puerto Vallarta nchini Mexico ambapo mataifa yataangazia ushirikiano wa uhamiaji na maendeleo ya kibinadamu miongoni mwa masuala mengine.

Kwa muda wa siku mbili za mkutano huo mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yatakuwa na mazungumzo yatakayofuatwa na maajadiliano kati ya nchi yatakayoangazia zaidi uhamiaji na maendeleo , haki za binadamu kwa wahamiaji wote na uhamiaji usio na wakati. Mkuu wa tume atafungua mkutano huo kuadimisha miaka ishirini ya kulinda haki za wafanyakazi wahamiaji na watu wa familia zao ambapo pia atasoma hotuba ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati wa siku ya pili ya mkutano huo