Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola bilioni 100 kwa mwaka zitapatikana kukabili mabadiliko ya hali ya hewa ifikapo 2020:UM

Dola bilioni 100 kwa mwaka zitapatikana kukabili mabadiliko ya hali ya hewa ifikapo 2020:UM

Itawezekana kukusanya dola bilioni 100 kwa mwaka ili kusaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, gesi za viwandani na kuimarisha maendeleo endelevu.

Hayo yamo kwenye hitimisho la ripoti ya kundi la ngazi za juu la la ushauri la Umoja wa Mataifa kuhusu kufadhili masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa.Wenyeviti wa kundi hilo ni Meles Zenawi waziri mkuu wa Ethiopia na norway.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akizungumza kwenye uwasilishaji wa ripoti hiyo amesema ana matumaini kwamba fedha hizo zitapatikana.

(SAUTI YA BAN Ki-MOON)