Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa wahisani wa kujenga amani wafanyika UM

Mkutano wa wahisani wa kujenga amani wafanyika UM

Mkutano wa wadau wa mfuko wa masuala ya jujenga na kudumisha amani unafanyika leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New york.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema mfuko huo ni moja ya nguzo muhimu kwa Umoja wa Mataifa katika kazi zake za kuleta amani. Amesema mkutano wa leo ni fursa nzuri na muhimu ya kufikiria hatua zilizofikiwa na mfuko huo katika mwaka wake wa kwanza na jinsi gani ya kuimarisha mchango wake katika masuala ya amani.

Ban amewataka wadau katika mkutano huo kuongeza msaada wa kifedha kutunisha mfuko huo kwani amesema kuleta amani sio kazi rahisi.

(SAUTI BAN Ki-MOON)

Ban amesema kuhakikisha machafuko hayatokei tena mtazamo wa amani wa kimataifa unahitajika , kwani jumuiya ya kimataifa ina jukumu kubwa la kuzisaidia nchi kusonga mbele, kujenga amani na maendeleo.