Chama cha msalaba mwekundi yaanzisha mkakati wa dharura kuwasaidia waathirika wa mafuriko Sudan KusinI

29 Oktoba 2010

Chama cha msalaba mwekundu dunaini kimeanzisha mkakati wa dharura wenye shabaya ya kukusanya zaidi ya dola za kimarekani milioni 2.4 kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mafuruko Sudan ya Kusini, wanaofikia zaidi ya watu 50,000.

Watu hao wapo katika hali mbaya kutokana na kuendelea kukosa makazi, maji safi na salama na huduma nyingine za dharura za afya. Tayari chama cha msalaba mwengundu cha Sudan kimepelekwa wafanyakazi wa kujitolea 2,400 ambao wameendelea na kazi ya ukoaji na utoaji misaada.

Kiwango kikubwa cha mvua kilichoanza kunyesha kuanzia mwezi July kimeleta madhara pia kwenye maeneo mingine kama kuharibu miundo mbinu, mazingira. Hilo ni pigo kubwa kwa watu wa eneo hilo ambao wameanza kuchomoza upya baada ya kushuhudia machafuko ya muda mrefu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter