Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali zakubaliana mpango wa kuzuia kupotea kwa mali asili

Serikali zakubaliana mpango wa kuzuia kupotea kwa mali asili

Baada ya karibu miaka ishirini ya mazungumzo na mijadala serikali kutoka sehemu mbali mbali duniani hii leo zimeafikia makubaliano mapya ya kusimamia mali asili yenye umuhimu wa kiuchumi duniani .

Pia yanatoa mwelekeo wa jinsi manufaa yanayopatikana kwa mfano kutoka kwa jenetiki za mimea na kuwa bidhaa ya kuuuzwa kama vile madawa, yanaweza kugawa kati ya nchi au jamii ambazo zimetunza mali hiyo. Katibu mkuu wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP Achim Steiner amesema kuwa hii ni siku ya kusherehekea baada ya kupatikana kwa jibu la kukabiana na kupotea kwa baolojia anuai.