Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamia ya wasomali waendelea kukimbilia Kenya

Mamia ya wasomali waendelea kukimbilia Kenya

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa linasema kuwa hali inaendeea kuwa mbaya kaskazini mwa Kenya baada ya mamia ya wasomalia kuendelea kuingia nchini Kenya wakikimbia mapigano kati wanamgambo wa Al-Shabaab na kundi la Ahlu Sunna Wal Jamaa linaloegemea upande wa serikali ya mpito ya Somali kwenye mji wa mpaka wa Beled Hawo. George Njogopa na taarifa kamili

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Hali siyo ya kutia matumani na kumeshuhudiwa zaidi ya wakimbizi 7,100 wakiranda randa karibu na mpaka baina ya Kenya na Somalia. Wengi wao ni wanawake, watoto na wazee ambao hali ya afya zao zimezidii kudhoofika siku baada ya siku. Lakini wengi walilazimika kuweka kambi ya muda katika eneo lililopo karibu na kituo cha mpakani wakati mapigano hayo yalizuka upya October 17.

Hapa jana gari moja lilikuwa likimilikiwa na taasisi ya kiislamu ya utoaji misaada lilishambuliwa wakati likiwa kwenye harakati ya kutoa misaada kwa wakimbizi hao. Hatua imefanya shughuli za utoaji wa misaada ya kiutu kusimama lakini ikarejeshwa tena baada ya serikali ya Kenya kutoa ulinzi mkali.

Iwapo mapigano hayo yataendelea tena katika eneo hilo la Beled Hawo, wasiwasi uliopo ni kwamba maisha ya wakimbizi wengi yatakuwa hatarini. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR imeitolea mwito serikali ya Kenya kuanza kuwatafutia maeneo wakimbizi hao kwani kuwaacha kusalia eneo moja kunaweza kuleta maafa zaidi