Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya wakimbizi wa DRC warejea nyumbani kwa hiari kutoka Zambia

Maelfu ya wakimbizi wa DRC warejea nyumbani kwa hiari kutoka Zambia

Karibu wakimbizi 47,000 raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambao wamekuwa wakiishi nchini Zambia wamerejea nyumbani kwa hiari kwenye mpango ulioanzishwa miaka minne iliyopita na shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR.

Kundi la mwishio la wakimbizi 131 liliondoka nchini Zambia siku ya Jumatano wiki hii na kuelekea katika mkoa wa Katanga ulio kusini mwa DRC. Msemaji wa UNHCR Adrian Edwards anasema kuwa shirika hilo litafunga kambi mbili ambazo zimekuwa makao ya wakimbizi hao na kuzikabidhi kwa serikali ya Zambia.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)

UNHCR inasema kuwa wakimbizi wengine 2000 kutoka DRC ambao hawakutaka kurejea nyumbani wamepelekwa katika eneo la Meheba lililo kaskazini magharibi mwa Zambia. UNHCR pia imerejelea mpango wa kuwarejesha nyumbani kwa hiari wakimbizi wa DRC wanaoishi nchini Burundi