Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake lazima wapewe umuhimu katika jamii:UM

Wanawake lazima wapewe umuhimu katika jamii:UM

Mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa nchi kuwapa umuhimu wanawake kulingana na mipango ya kijamii hususan kwenye masuala ya kijamii.

Magdalena Sepulveda ameifahamisha kamati ya UM inayohusika na majukumu ya kijamii , kitamaduni na kibinadamu kuwa kuwashirikisha wanawake kwenye masuala ya kijamii kunachangia wao kushiriki kwenye miradi ya uchumi na kuwasaidia kuwa na mapato siku zao za uzeeni.

Amesema kuwa mara nyingi wanawake hujipata kwenye umaskini kwa sababu ya kubaguliwa na kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia na kutoa wito kwa hatua kuchukuliwa kafanikisha lengo la kumaliza umasikini ifikapo mwaka 2015. Hata hivyo ameonya kuwa mipango ya kijamii hususan inayowalenga wanawake kama haitatumika kwa njia inayofaa v inaweza kuchangia kutokuwepo kwa usawa.

.