Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wanaendelea kuwa na jukumu muhimu katika ulinzi wa amani

Wanawake wanaendelea kuwa na jukumu muhimu katika ulinzi wa amani

Wanawake wanaendelea kuwa na jukumu muhimu katika juhudi za kuleta amani amesema Bi Michelle Bachelete mkuu wa kitengo kipya cha Umoja wa Mataifa cha wanawake UN-Women.

Akizungumza kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa hii leo wakati wa maadhimisho ya 10 ya azimio namba 1325 la jukumu la wanawake katika amani na usalama, amesema Umoja wa Mataifa umechukua hatua muhimu kuhakikisha kwamba wanawake wanashiriki katika kufanya maamuzi na juhudi za kuleta amani.

Bi Bachelet ameitaja Sudan kama mfano wa ongezeko la juhudi za wanawake katika masuala ya kulinda amani.

(SAUTI MICHELLE BACHELET)

Amesema katika mwezi huu, wanawake 90 maafisa washauri wa polisi kutoka Rwanda wamepelekwa kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa na wa Afrika Darfur ili kuhudumu kama washauri wa masuala ya jinsia na ukatili dhidi ya wanawake na pia kuwalinda watoto.

Sierra Leone ambayo iliruhusu kuwa na askari wanawake 2008 imepeleka wanawake saba walinda amani Sudan akiwemo mwanamke mmoja Brigedia jeneral na muda si mrefu watapeleka wengine 20 zaidi.