Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miezi michache kabla ya kura ya maoni Sudan kuna masuala ya kutatuliwa:Ban

Miezi michache kabla ya kura ya maoni Sudan kuna masuala ya kutatuliwa:Ban

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa wakati nguvu za kisiasa nchini Sudan zinapoelekezwa kwa kura ya maoni bado tofauti zilizopo kati ya pande zilizo kwenye makubaliano ya amani zinaendelea kuchelewesha maandalizi ya kura hizo.

Akiwasilisha ripoti kuhusu Sudan mbele ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Ban amesema kuwa kufuatia kubuniwa kwa tume ya kura ya maoni kusini mwa Sudan mnamo tarehe 28 mwezi Juni mzozo umeibuka kati ya wanachama wa makubaliono ya amani kuhusu ni nani angeteuliwa kuhudumu kama katibu wa tume hiyo .

Mzozo huo umebaki bila jibu kati ya miezi ya Julai na Agosti hali ambayo imezuia tume hiyo kuendeleza mipango yake wakati huo wote. Lakini serikali ya Sudan kwa upande wake imesema iko tayari kutatua matatizo na kasoro zilizopo

(SAUTI SUDAN)