Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takwimu ni kiini cha kuleta mabadiliko:UNICEF

Takwimu ni kiini cha kuleta mabadiliko:UNICEF

Wataalamu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wametoa wito wa kuzingatia umuhimu wa takwimu katika kuunda sera na miapango ya maendeleo ili kuboresha maisha ya wanawake na watoto duniani.

UNICEF imetoa wito huo katika kuandhimisha siku ya takwimu duniani na kusema inaunga mkono na kusaidia nchi mbalimbali katika ukusanyaji, uhakiki na matumizi ya takwimu katika kuangalia hali ya wanawake na watoto hususan katika nchi zinazoendelea.

UNICEF inasema takwimu hizo zinatumika na shirika hilo na mengine kubaini matatizo, kutathimini mipango na kufuatilia hatua zinazopigwa katika kuelekea kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia.

Shirika hilo limeongeza kwamba bila takwimu kama hizo serikali, jumuiya ya misaada ya kimataifa na waandishi wa habari watakuwa na wakati mgumu hasa kuarifu kuhusu matatizo na changamoto zinazowakabili wanawake na watoto.