Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wafanya ziara kabla ya mazungumzo Sahara Magharibi

UM wafanya ziara kabla ya mazungumzo Sahara Magharibi

Ujumbe unaoongoza jitihada za Umoja wa Mataifa za kusaidia kupata suluhu la hali ya sahara magharibi unatarajiwa kusafiri kwenda eneo hilo kabla ya awamu nyingine ya mikutano inayotarajiwa kuandaliwa mwezi Novemba mwaka huu.

Mjumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Christopher Ross anatarajiwa kuwasili eneo hilo baadaye mwezi huu kwa majadiliano kati ya pande husika zikiwemo Morocco na eneo la Frente Polisario na mataifa jirani ya Algeria na Mauritania.

Mazungumzo hayo yanaandaliwa kuambatana na uamuzi wa baraza la usalama la UM wa mwaka 1871 uliotoa wito kwa pande husika kuendelea na mazunguzo hayo pasipo vikwazo ili kupata makubaliano ya kudumu. Mapigano yalizuka kati ya Morocco na eneo la Frente Polisario baada ya utawala wa kikoloni wa Hispania katika eneo la Sahara Magharibi kumalizika mwa 1976.

Morocco imekuwa na mpango wa kulitawala eneo la Frente Polisario huku eneo hilo lilitaka kufanyika kura ya maoni na hata kuwa huru.