Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanajeshi zaidi wa UM wamewasili Ivory Coast

Wanajeshi zaidi wa UM wamewasili Ivory Coast

Umoja wa Mataifa unagawa vitambulisho na kadi za kupigia kura katika miji mikuu yote ya Kaskazini inayodhibitiwa na waasi ya ya kusini inayodhibitiwa na serikali katika maandalizi ya uchaguzi unaotarajiwa kumaliza mgawanyiko uliosababishwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya 2002.

Wakati huohuo wanajeshi wa kwanza 500 wa nyongeza wamewasili jana nchini humo ili kuongezea nguvu vikosi 8650 vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa UNOCI na kusaidia masuala ya usalama wakati wa uchaguzi.

Duru ya kwanza ya upigaji kura katika uchaguzi huo uliochelewa kwa muda mrefu imepangwa kufanyika tarehe 31 ya mwezi huu na kufuatiwa na duru ya pili tarehe 28 Novemba kama hakuna mshindi dhahiri kwenye duru ya kwanza. Kwa mujibu wa msemaji wa UNOCI Mamadoun Toure wanajeshi wengine zaidi watawaili wiki ijayo na watasaidia pia katika usafirishaji wa masanduku ya kura .

Ameongeza kuwa kutakuwa na semina maalumu na waangalizi wa kimtaifa wa uchaguzi itakayoongozwa na mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu Ban Ki-moon nchini humo Y.J.Choi kuwaelewesha kuhusu mchango wa UNOCI katika mchakato wa uchaguzi.