Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya ICC yatoa uamuzi wa hatma ya Lubanga

Mahakama ya ICC yatoa uamuzi wa hatma ya Lubanga

Kitengo cha rufaa cha mahaka ya kimataifa ya uhalifu ICC iliyoko The Hague Uholanzi leo imetoa uamuzi kuhusu hatma ya Thomas Lubanga. Sonia Robla ni msemaji wa ICC anafafanua kuhusu uamuzi uliotolewa.

(SAUTI YA SONIA ROBLA)

Julai 8 mwaka huu kitengo cha kesi kiliamua kwamba kesi ya Lubanga ifutwe na aachiliwe huru kwa sababu waliamini haki haiwezi kutendeka kutokana na upande wa mashitaka kushindwa kutekeleza maamuzi ya mahakama ya kutoa taarifa za mashahidi 143 na tarehe 15 July wakamua Lunganga aachiliewe lakini upande wa mashitaka ukakata rufaa.

Bwana Thomas Lubanga anashutumiwa kwa makosa ya uhalifu wa vita na kuwatumia watoto vitani kwenye jimbo la Ituri kati ya Septemba 2002 na Agosti 2003.