Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlinda amani wa UM atekwa nyara Darfur Sudan

Mlinda amani wa UM atekwa nyara Darfur Sudan

Mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID kwenye jimbo la Darfur Sudan unashirikiana na serikali ya nchi hiyo ili kuachiliwa kwa raia mlinda amani aliyetekwa nyara kutoka maeneo ya UNAMID jana Alhamisi.

Mtu huyo alitekwa wakati ujumbe wa baraza la usalama la usalama ukifanya ziara kwenye mji mkuu wa Darfur El-Fasher. Kwa mujibu wa msemaji wa UNAMID Kemal Saiki , uongozi wa Sudan umeshaanza mara moja kumsaka mateka huyo.

Amesema kundi la watu wane au watano waliokuwa na silaha waliingia kwenye nyumba ambayo walikuwa wanaishi wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa jana usiku na kuwateka watu wawili, waliwafunga, lakini walifanikiwa kuondokana na mmoja wao kwa kutumia gari la UNAMID lililokuwa hapo. Hali ya usalama imeelezewa kuwa bado ni tete kwenye jimbo la Darfur.