Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakaribisha tangazo la mshindi wa Nobel kutoka Uchina

UM wakaribisha tangazo la mshindi wa Nobel kutoka Uchina

Tangazo la mshindi wa tuzo ya nobel ya mwaka 2010 kwenda kwa mfungwa wa Uchina limekaribishwa na umoja wa Mataifa.

Katika taarifa yake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ushindi wa Liu Xiaobo ni kutambua ongezeko la kimataifa la kutaka kuimarisha haki za binadamu na utamaduni kote dunian. Ban amekuwa akisisitiza umuhimu wa haki za binadamu sambamba na maendeleo, amani na usalama kama ni nguzo tatu kubwa za kazi za Umoja wa Mataifa.

Ban ameongeza kuwa ama imani tofauti zozote zilizojitokeza kuhusu umamuzi wa kumtunukia tuzo Xiaobo hazitotia dosari ajenda ya kimataifa ya kugania haki za binadamu au nguvu na uwezo wa tuzo hiyo.

Naye mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay

anakaribisha ushindi huo kwa kile alichosema wanaharakati wa haki za binadamu wa jukumu muhimu nchi Uchina na kuongeza kuwa wachagizaji kama Xiaobo wanaweza kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya Uchina.

Serikali ya Uchina imekasirishwa na tangazo hilo ikisema litatia doa uhusiano baina ya Uchina na Norway ambayo ni maskani ya kamani ya Nobel. Xiaobo ameshinda tuzo hiyo licha ya kutumia kifungo cha miaka 11 kwa kuikasirisha serikali.