Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umeidhinisha mikakati ya kimataifa kuwalinda nguva

UM umeidhinisha mikakati ya kimataifa kuwalinda nguva

Mkutano wa kimataifa uliandaliwa na Umoja wa Mataifa wiki hii nchini Abu Dhabi kuhusu nguva , umepitisha mkakati maalumu kuwalinda viumbe hao adimu.

Mkutano huo uliofanyika chini ya mkataba wa kuwalinda viumbe na wanyama pori wanaohama UNEP/CMS) umewaleta pamoja serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, mashirika ya kimataifa na wataalamu. Mkutano huo umejadili njia za muafa na suluhu ya kuwalinda nguva wanyama pekee wanyonyeshao wanaoishi majini.

Nguva wamelelezewa kuwa katika hatari ya kutoweka kabisa katika mika 40 ijayo. Na baadhi ya njia zilitoidhinishwa kuwalinda viumbe hao ni vifaa na dawa vitakavyosaidia kutovuliwa viumve hao na kuongeza uzalishaji wao.

Mambo yanayochangia kupunguza idadi ya viumbe hao ni pamoja na uvuvi haramu, ujangiri, kuumizwa na meli, na kutoweka kwa majani baharini ambayo ni makazi ya nguva.