Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wajadili biashara na uchumi unaojali mazingira:UNCTAD

Wataalamu wajadili biashara na uchumi unaojali mazingira:UNCTAD

Wataalamu kwenye mkutano wa kimataifa uhusuo uchumi unaozingatia mazingira, wamesema msukumu wa kimataifa unaweza kuwa chachu mpya kwa maendeleo endelevu na yanayojumuisha pande zote husika.

Wataalamu hao wanasema msukumo huo utasaidia kusambaza teknolojia, uzoefu na faida. Mkutano huo wa siku mbili ambao pia unaangalia biashara na athari katika maendeleo endelevu umeandaliwa kama maandalizi ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo endelevu unaotarajiwa kufanyika mwaka 2012 ambao mada kuu mbili zitazingatiwa ikiwemo uchumia unaojali mazingira na kutokomeza umasikini.

Katibu Mkuu wa UNCTAD Supachai Panitchpakdi akizungumza kwenye mkutano huo mjini Geneva amesema masuala ya mazingira hayawezi kuepukika, ameongeza kuwa juhudi zinahitajika kuwezesha ukuaji wa uchumi ambao hauharibu mazingira na nchi masikini zinahitaji msaada zaidi kufanikisha hilo.

Ameongeza kuwa biashara inaweza kuwa nyezo muhimu katika mabadiliko ya kuingia uchumi unajali mazingira lakini biashata tuu bila msaada zaidi haiwezi kuzikwamua nchi masikini. Amesema ili kukabiliana na mzigo wa matatizo ya mabadiliko ya hali ya hewa mfumo madhubuti wa kushirikiana unahitajika.

Naye Sha Zukang mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu katika masuala ya kijamii na uchumi amesema maendeleo endelevu ni dhana muhimu lakini inamaanisha nini na jinsi gain inawezekana ndilo suala linalohitaji ufumbuzi, kwani kbado kuna kazi kubwa kutimiza hilo.