Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waunga mkono ukusanyaji bora wa kodi kwa nchi masikini

UM waunga mkono ukusanyaji bora wa kodi kwa nchi masikini

Umoja wa Mataifa umetoa zingatio lake kuunga mkono mkutano unaojadilia mbinu za kisasa ambazo zinaweza kuchangia pakubwa katika uimarishwaji wa vyanzo vya uletaji maendeleo kwa nchi zinazoendelea.

Mkuano huo ambao unafanyika katika ofisi za Umoja wa Mataifa Lisbon, Ureno,unajaribu kubainisha vipaumbele vinavyopaswa kuwekwa na nchi zinazoendelea ili kufukia shabaya ya kukuza uchumi wake wa ndani na maingiliano zaidi ya kiuchumi.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mshauri wa Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya Afrika Cheick Sidi Diarra, amesema mkutano huo unakusudia kuweka maazimio ambayo yatafikishwakwenye mkutano wa nne wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika mwaka ujao 2011 Istanbul kujadilia hali za nchi zinazoendelea.