Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wasisitiza matumizi ya tovuti ili kuchagiza maendeleo

UM wasisitiza matumizi ya tovuti ili kuchagiza maendeleo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amesisitiza haja ya matumizi ya mtandao wa internet kwa njia ya broadband ili kuchagiza hatua za kufikia malengo ya maendeleo, na hasa kupunguza umasikini na kuinua kiwango cha uchumi hususan katika nchi masikini.

Ban amesema uzoefu umeonyesha kwamba matumizi ya teknolojia ya broadband yamesaidia kuchepusha mipango ya kufikia malengo ya maendeleo ya milenia . Ban ameyasema hayo katika ujumbe maalumu kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa jumuiya ya kimataifa ya mawasiliano ITU ambao umeanza leo mjini Guadalajara nchini Mexico.

Ameongeza kuwa internet inaimarisha biashara, uchumi na hata elimu, huku tiba kwa njia ya teknolojia imeboresha afya za watu, na vitu kama mitambo ya satellite imetumika kushughulikia matatizo na mabadiliko ya hali ya hewa. Mwezi uliopita tume ya broadband kwa ajili ya maendeleo, kundi la maafisa wa serikali mbalimbali, wafanya biashara na wataalamu wa mtandao walikutana pamoja chini ya usimamizi wa ITU na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO na kutoka na muongozi ,jambo ambalo Ban amesema ni la muhimu na yuko tayari kushirikiana nao kutekeleza muongozo huo.

Amesema kwa sasa kuwa watu bilioni 5 wanaotumia simu za mkononi duniani na watu takribani bilioni mbili waliounganishwa na mtandao wa internet ikidhihirisha juhudi za ITU, nchi wanachama na sekta husika zinavyoshirikiana kwa ajili ya kuleta maendeleo , kwa njia huru nay a uwazi.