Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi ya cabon yapungue kunusuru hali ya hewa

Matumizi ya cabon yapungue kunusuru hali ya hewa

Wakati huohuo viongozi wa mashirika ya kimataifa yenye ushawishi mkubwa na mashirika muhimu ya kimataifa ya mazingira leo wanatarajiwa kutoa wito kwa serikali kuhakikisha mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa utakaofanyika Cancun unakuwa wa mafanikio.

Katika mkutano huo unaohudhuriwa pia na mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP Achin Steiner mjini Geneva, shirika la biashara kwa ajili ya mazingira B4E litazungumza kwa niaba ya mashirika mengine ya biashara ya kimataifa ili kuzichagiza nchi kujitahidi kupunguza matumizi ya gesi ya cabon katika mifumo ya biashara kabla ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa utakaofanyika Cancun Mexico.

Mkutano wa Cancun utawaleta pamoja wakuu wan chi mbalimbali, mashirika ya kimataifa, wadau wa mazingira na biashara na Umoja wa Mataifa, na utaanza Nevemba 29 hadi December 10.