Skip to main content

Vifo vya malaria vinaweza kukomeshwa ifikapo 2015:UM

Vifo vya malaria vinaweza kukomeshwa ifikapo 2015:UM

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya mipangilio ya sera Robert Orr amesema kuwa hata kama kuna hali mbaya ya uchumi duniani jitihada mpya zinazofanywa na serikali zinaonyesha matumani ya kupunguza vifo vinavyosababishwa na Ugonjwa wa malaria ambao kwa sasa vinawaua watu milioni moja kila mwaka kote duniani na kuukomesha ugonjwa huo ifikapo mwaka 2015.

Orr ametaja kujitolea kwa mataifa ya ufaransa , Canada , Norway na Japan katika kuchangia fedha kwa mpango wa UM wa mataifa unahudumia magonjwa ukiwemo wa Ukimwi , kifua kikuu na malaria.

Bwana Orr pia ameutaja kuwa wenye mafanikio mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa wa malengo ya maendeleo ya milenia uliowaleta pamoja jumla ya viongozi 139 katika juhudi za kuunga mkono jitihada zenye lengo la kuangamiza umaskini na njaa , vifo vya watoto wachanga na magonjwa itimiapo mwaka 2015.