Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya mama mwaka huu pia ni miaka 50 tangu kuanza kutumika tembe za uzazi

Siku ya mama mwaka huu pia ni miaka 50 tangu kuanza kutumika tembe za uzazi

Tarehe Tisa May ambayo ni siku ya mama ulimwenguni pia imesadifiana na kuazimishwa kwa miaka 50 tangu tembe za kuzuia uja uzito kuidhinishwa nchini Marekani.

Utumiaji wa tembe hiyo umeongezeka maradufu na kwa hivyo kuwapa wanawake uwezo wa kusimamia uzazi wao na kuwapa nafasi ya kufanya maamuzi ya maswala ya uzazi. Licha kuongezeka kwa teknolojia, bado tembe ndio inayotumiwa kuliko aina nyingine za kuzuia mimba.

Japo matumizi ya tembe yameongezeka huku kukiwa na takribani wanawake miliono mbili wanaotumia, kiasi sawa na idadi ya akina mama duniani ambao hawana fursa ya kuchagua mbinu ya kuzui mimba.