Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuna imani tutazidi asilimia 50 katika malengo ya milenia:Kenya

Tuna imani tutazidi asilimia 50 katika malengo ya milenia:Kenya

Pamoja kwa kwamba malengo yote ya maendeleo ya milenia ni muhimu Kenya inasema malengo yanayowahusu wanawake yamepewa uzito mkubwa.

Waziri wa jinsia watoto na maendeleo ya jamii wa Kenya Dr Naomi Shaaban akizungumza na mkuu wa Idhaahii wakati wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa tathimini ya hatua zilizopigwa kufikia malengo ya maendeleo hapo 2015 amesema wana imani kubwa kwamba watazidi asilimia 50 katika kutimiza malengo hayo.

Kwa sasa elimu kwa mtoto wa kike, kuwapa fursa wanawake katika ngazi za maamuzi, kuwapa nafasi za kujikwamua kiuchumi yanakaribia asilimia 50. Ungana nao katika mahojiano haya .