Skip to main content

Gharama za juu za chakula ni mada katika mkutano Roma

Gharama za juu za chakula ni mada katika mkutano Roma

Hofu ya kupanda kwa bei za chakula katika soko la kimataifa ni jambo linalojadiliwa katika mkutano wa kimataifa ulioandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO.

Bei za chakula zimesalia kuwa juu duniani kote kufuatia mdororo wa uchumi, Urusi kupiga marufuku usafirishaji wa ngano na mafuriko yaliyosambaratisha eneo la kilimo nchini Pakistan na Uchina.

Akizungumza mjini Roma Italia kwenye mkutano huo mkurugenzi mkuu wa FAO Jacques Diouf amesema soko la dunia bado liko njia panda.

(SAUTI YA JACQUES DIOUF)

Ongezeko la bei limekumba kuanzia ngano hadi nafaka zingine na zaidi. Takwimu za bei ya chakula za FAO zimefikia kiwango cha juu kabisa tangu Septemba 2008. Masoko yanayumba na hali hii huenda ikaendelea.

Viongozi wa Afrika wametaka ujumbe wa kudumu kwenye baraza la usalama kwa bara hilo.