Skip to main content

Saratani inakatili maisha ya mamilioni kila mwaka:WHO

Saratani inakatili maisha ya mamilioni kila mwaka:WHO

Wataalumu wa saratani kutoka kote duniani wamehitimisha mkutano wao mjini Vienna Austria uliokuwa ukijadili ongezeko la matatizo ya saratani katika nchi zinazoendelea.

Katika mkutano huo wa siku mbili uliohudhuriwa na wawakilishi wa serikali, wataalamu wa afya, na watafiti imebainika kuwa matatizo ya saratani yanaongezeka duniani na tatizo ni kubwa zaidi katika nchi zinazioendelea. Margareth Chan ni mkurugenzi wa shirika la afya duniani WHO,

(SAUTI MARGARETH CHAN)

Chan ambaye alikuwa akizungumza katika kufunga mkutano huo amesema Sekta ya afya ya nchi hizo imejikuta ikielemewa na matatizo hayo ambayo yametoka katika nchi tajiri na kuahamia zile masikini. Amesema mambo matatu yamechangia ongezeko la saratani katika nchi zinazoendelea ,uzee, ukuaji wa miji usio na mipango na utandawazi wa kufuata maisha yasiyozingatia misingi ya afya.