Baraza Kuu la UM limeanza rasmi mjadala leo kuhusu masuala mbalimbali yanayoikabili dunia na UM ukiwa na jukumu kubwa:

Baraza Kuu la UM limeanza rasmi mjadala leo kuhusu masuala mbalimbali yanayoikabili dunia na UM ukiwa na jukumu kubwa:

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo linaanza mjadala katika mkutano wake mkuu wa kila mwaka wa viongozi wa dunia mjini New York.

Zaidi ya wakuu wa nchi na wawakilishi wa serikali 130 watahutubia baraza hilo na kuainisha mtazamo wao katika masuala mbalimbali yanayoitia mashaka dunia kwa sasa. Mkutano huo wa 65 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapa New York unatoa fursa kwa viongozi hao kueleza pia maoni yao katika mambo wanayoyaona kuwa ni muhimu.

Kwa kawaida Brazil ndio huwa kinara wa kuanza mjadala huo, ikifuatiwa na Marekani ambapo Rais Barack Obama atahutubia baraza hilo kwa mara ya pili.

Mjadala huo unafuatia kukamilika kwa mkutano wa tathimini ya malengo ya maendeleo ya milenia jana usiku. Na mjadala huu unatarajiwa kudumu kwa zaidi ya wiki moja.