UM ni muhimu katika kukabili matatizo ya kimataifa:Leuthard

UM ni muhimu katika kukabili matatizo ya kimataifa:Leuthard

Rais wa Uswis amesema Umoja wa Mataifa ni kiini cha kusaidia kukabiliana na matatizo yanayoikabili dunia.

Rais Doris Leuthard akizungumza katika mjadala wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa hii leo ameonya kwamba Umoja wa Mataifa usijegeuka kile alichokiita kama mnara wa kihistoria. Amesema Umoja huo unahitaji kuwa shirika linaloweza kusimama katika hali zote.

Ameongeza kuwa UM ndio chombo pekee duniani kinachoweza kupunguza tofauti zilizopo na kurejesha utengamano baina ya mataifa. Amesisitiza kuwa, hata hivyo kila nchi mwanachama lazima iyaweke masilahi yake baada ya yale ya pamoja kwa faida ya wote.