Skip to main content

Baraza kuu la UM limeanza leo mjadala kuhusu masuala mbalimbali

Baraza kuu la UM limeanza leo mjadala kuhusu masuala mbalimbali

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa leo limeanza mjadala wa masuala mbalimbali ikiwemo utawala wa kimataifa.

(SAUTI YA BAN GA)

Hiyo ni sauti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akizungumza katika ufunguzi rasmi wa mjada wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa ulioanza leo mjini New York. Anasema wakati tumekusanyika pamoja kwa mshikamano leo tutambue huu ni wakati wa kuungana kwa ajili ya kupiga hatua ,kufanya kazi kwa bidii na kuleta matunda. Matunda yanayohitajika kwa watu wanayoyahitaji zaidi na Umoja wa Mataifa pekee ndio unaoweza kusaidia kufanya hivyo. Ban amesema hizi sio ndoto ni fursa zilizopo ndani ya uwezo wetu kuzitekeleza, la msingi ni kushikama na kufanya kazi pamoja.

Mjadala huo unaofanyika katika kikao cha 65 cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa unajadili masula mbalimbali yanayoisumbua dunia hivi sasa. Leo katika siku ya kwanza ya mjadala unaojumuisha wakuu wa nchi na wawakilishi wa serikali zaidi ya 130 mada kuu ni utawala wa kimataifa. Akizungumza katika mjadala huo waziri wa mambo ya nje wa Brazili Celos Luiz Nunes Amorim akimwakilisha Rais Lula Da Silva amesema Brazil inachukua jukumu la utawala wa kimataifa kwa kuisaidia Afrika

(SAUTI CELOS AMORIM)

Naye Rais Barack Obama wa Marekani moja ya mataifa yenye nguvu na ushawishi duniani amezungumzia masuala mengi ikiwemo usalama, kutokomeza nyuklia, umasikini, maradhi, uchumi na kikubwa zaidi muafaka wa Israel na Palestina

(SAUTI BARACK OBAMA ISRAEL)

Kuhusu Afrika Barack Obama amepongeza matumaini yaliyofikiwa Kenya kwa kupata katiba mpya na kwa bara zima amesema haoni ni kwa nini siku zote liwe mpokeji wa bidhaa toka nje.

(SAUTI OBAMA AFRICA)

Miongoni mwa viongozi wa Afrika waliopaza sauti zao kueleza madukuduku yao katika mjadala huo ni Rais Bingu wa Mutharika wa Malawi akizungumzia suala hilo hilo la Afrika amesema miaka mitano kuanzia sasa tatizo la chakula Afrika wanataka liwe historia

(SAUTI BINGU MUTHARIKA)

Na Rais Mwai Kibaki wa Kenya akigusia utawala wa kimataifa amesema

(SAUTI MWAI KIBAKI)

Majada huu utaendelea kwa zaidi ya juma zima na viongozi na wawakilishi wote watapata nafasi ya kuelezea masuala wanayodhani ni muhimu na yanayoisumbua dunia kwa sasa.