Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Liberia ametoa wito wa kuwa na uchumi unaotoa ajira:

Rais wa Liberia ametoa wito wa kuwa na uchumi unaotoa ajira:

Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf ametoa wito wa kukua kwa uchumi unaotoa ajira na hususan kwa vijana, masikini na wanawake.

Akizungumza kwenye mkutano ambapo viongozi wa dunia waliokusanyika mjini New York wakiendelea kutoa tathimini ya hatua walizopiga katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia kwa kupunguza umaskini na njaa na kuimarisha afya za watu ifikapo 2015 Bi Sirleaf amesema malengo ni ya kimataifa lakini athari zake ni za kitaifa.

Amesema wakati tukitathimini hatua zetu katika mwaka huu 2010 lazima tutambue haja ya uchumi utakaowajumuisha wote. Tunahitaji ukuaji wa haraka, imara na unaojitosheleza, ambao utatoa ajira hasa kwa vijana na sekta ambazo zitawanufaisha masikini na kutoa fursa kwa wanawake.