Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa UM kuhusu malengo ya milenia unaendelea kujadili njia za kukabili matatizo ya dunia:

Mkutano wa UM kuhusu malengo ya milenia unaendelea kujadili njia za kukabili matatizo ya dunia:

Mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kukabiliana na umasikini leo umeingia siku ya pili kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York.

Mkutano huo ulianza jana kwa ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akisema malengo ya milenia yanaweza kufikiwa. Amesema hatua kubwa imepigwa katika masuala mengi ikiwemo uandikishaji watoto shuleni, upatikanaji wa maji safi na udhibiti wa maradhi. Lakini ameongeza kuwa bado juhudi zaidi zinahitajika. Ameongeza kuwa bado kuna watu wanakabiliwa na njaa duniani, akisema ni kashfa kubwa kwamba watu kwa mabilioni wanalala bila kula.

Viongozi mbalimbali wamezungumzia hatua walizopiga katika nchi zao na leo Jumanne miongoni mwa watakaozungumza ni Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran na Hugo Chaves wa Venezuela.