Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza kuu la UM leo limeanza kujadili malengo ya maendeleo ya milenia(MDG's)

Baraza kuu la UM leo limeanza kujadili malengo ya maendeleo ya milenia(MDG's)

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa leo limeanza kujadili tathimini ya malengo ya maendeleo ya milenia

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Huyo ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akiwakaribisha wajumbe katika ufunguzi wa mkutano wa maelengo ya maendeleo ya milenia ambao ni sehemu ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa lililoanza mjada wake hii leo mjini New York.

Amesema malengo manane ya maendeleo ya milenia imekuwa ni hatua muhimu iliyopigwa, kwa pamoja tuliunda mikakati ya kutokomeza umasikini uliokithiri na kujiwekea malengo yanayowezekana na kwa muda maalumu.

Wakuu wa nchi na wawakilishi kutoka wanachama wote 192 wa Umoja wa Mataifa wanahudhuria mjadala huo wa kikao cha 65 cha Umoja wa Mataifa kinaojikita katika kutathimini hatua zilizopigwa katika kufikia malengo ya amaendeleo ya milenia hapo 2015. Naye raid wa baraza kuu la Umoja wa Mataika akizungumza kwenye mkutano huo Bwana Joseph Deiss amesema

(SAUTI YA JOSEPH DEISS)