Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa dunia wamekusanyika kweny UM kujadili MDG's

Viongozi wa dunia wamekusanyika kweny UM kujadili MDG's

Viongozi wa dunia wamekusanyika kwenye makao makuu ya UM kutoa msukomo wa kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.

Viongozi wa dunia wamekusanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York na wameanza mjada katika mkutano wa siku tatu wa kutathimini hatua zilizopigwa kufikia malengo ya maendeleo ya milenia MDG's.

Ikiwa imesalia miaka mitano tuu kabla ya muda wa misho uliowekwa kutimiza malengo hayo , viongozi hao wa dunia watajadili ni vipi na ni wapi wanatakiwa kuongeza juhudi zaidi katika kipindi kilichosalia ili kutokomeza umasikini, kupunguza njaa, kuzuia uharibifu wa mazingira, kuinua kiwango cha elimu, kuimarisha afya ya amama na mtoto na kufikia malengo mengine yaliyosalia. Na muda wa kufikia malengo hayo ni ifikapo 2015. Taarifa zaidi kuhusu mkutano huo zitakujia muda si mrefu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akiandika katika ripoti yake mapema mwaka huu alisema miaka 10 imepita tangu kuridhia azimio la malengo ya milenia na kuweka historia ya kupunguza umasikini kwa nusu hasa kwa kutekeleza malengo ya manane ya maendeleo kwa kipindi maalumu.