Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya maendeleo ya UM ikabiliane na changamoto:Ban

Kamati ya maendeleo ya UM ikabiliane na changamoto:Ban

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amewashauri wanachama wa kamati ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa kutumia maarifa zaidi yatakayohakikisha kuwepo kwa manufaa katika siku za usoni.

Kamati hiyo ilifanya mkutano wake wa kwanza kabisa kabla ya mkutano mkuu wa baraza la Umoja wa Matiafa. Kamati hiyo imepewa jukumu la kutafuta suluhu la njia za kuangamiza umaskini na kuzingatia utunzaji wa mazingira . Ban amesema kuwa itimiapo mwaka 2050 ulimwengu utakuwa na watu bilioni 9 mwaka ambao pia hewa inayochafua mazingira inastahili kupungua kwa siimia 50.

Kamati hiyo inaongozwa na marais Tarja Halonen wa Finland pamoja na Jacob Zuma wa Afrika kusini inawaleta pamoja waakilishi kutoka nchi tajiri na zile maskini. Mapendekezo ya kwaza ya kamati hiyo yatawasilishwa kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa mwishoni mwa mwaka 2011.