Skip to main content

Muogeleaji azunguka dunia kuchagiza malengo ya milenia

Muogeleaji azunguka dunia kuchagiza malengo ya milenia

Muongeleaji kutoka nchini Jamhuri ya Dominican amehitimisha ziara yake ya kuchagiza kuhusu malengo ya maendeleo ya milenia duniani kote.

Muongeleaji huyo Marcos Diaz jana Jumatano aliogelea kutoka mranara maarufun wa uhuru mjini New York Statute of Liberty hadi kwenye bustani iliyo mkabala na makao makuu ya Umoja wa Mataifa kukutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Muogeleaji huyo amemkabidhi Katibu Mkuu ujumbe alioukusanya kutoka kwa wananchi mbalimbali duniani. Tangu mwezi Mai mwaka huu Diaz ameogelea katika mabara matano ili kuchagiza watu kuunga mkono malengo ya maendeleo ya milenia. Akizungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa kuhusu nia yake diazi amesema

(CLIP MARCOS DIAZ)