Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amezindua ripoti ya mapungufu ya malengo ya milenia

Ban amezindua ripoti ya mapungufu ya malengo ya milenia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amezindua ripoti ya maalumu ya 2010 ya jopo la kuangalia mapungufu ya malengo ya maendeleo ya milenia.

Ban aliunda jopo hilo mwaka 2007 ili kutathimini hatua zinazopigwa katika kufikia malengo ya milenia.

Ripoti ya mwaka huu imejikita katika zaidi katika athari za mdororo wa uchumi, na inaonyesha kuwa matatizo hayo ya uchumi yamechangia upungufu mkubwa wa misaada, biashara na madeni. Pia umesababisha watu wengi kushindwa kumudu madawa na teknolojia.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Ban amesema ingawa msaada rasmi wa maendeleo uko katika kiwango cha juu hivi sasa bado kuna upungufu wa dola bilioni 20 za kukamilisha majukumu ya mwaka huu na Afrika inaongoza kwa upungufu wa dola bilioni 16. Hata hivyo amesema hivi sasa bishara imeanza kutengamaa, hatua kubwa imepigwa katika kuzifutia madeni nchi masikini, huku kupanda kwa gharama za madawa kunazidi kuongeza adha.