Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya kimataifa ya kulinda tabaka la ozoni kwa kusisitiza utawala na uwajibikaji

Leo ni siku ya kimataifa ya kulinda tabaka la ozoni kwa kusisitiza utawala na uwajibikaji

Leo ni siku ya kimataifa ya kulinda tabaka la ozoni . Kauli mbiu ya mwaka huu ni kulinda tabaka la ozoni, utawala na utekelezaji ndio nguzo.

Juhudi za kimataifa za kulinda tabaka hilo ambalo ni ngao inayolinda dunia kutokana na miale hatari ya jua zimetajwa kama mafanikio ambayo yamefaulu kuzuia kuharibiwa zaidi kwa tabaka hilo. Ripoti mpya iliyoandaliwa na karibu wanasayansi 300 imezinduliwa leo katika kuadhimisha siku hii na kusema makubaliano ya Montreal yamefanikiwa kulilinda tabaka la ozoni. Maelezo zaidi na Jason Nyakundi.

(RIPOTI JASON NYAKUNDI)

Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa kati ya vitu vinavyochangia kuharibika kwa tabaka hilo la ozone ni pamoja na gesi chafu huku makubaliono ya Montreal yakichangia manufaa makubwa kwa kupunguza mabadiliko ya hali ya hewa.  Ripoti hiyo iliyochapishwa na shirika la hali ya hewa duniani WMO kwa ushirikiano na shirika la mazingira la umoja wa mataifa UNEP inasema kuwa suala muhimu kwa sasa ni kulinda tabaka la ozone.

kwa siku zijazo na kuelewa zaidi athari za mabadiliko ya hali ya hewa Ripoti hiyo inaongeza kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yanatarajiwa kuwa na athari zaidi kwa tabaka la ozone kwa miaka kadha inayokuja huku shughuli za kibinadamu na gesi inayochafua mazingira vikitajwa kuchangia hali hii.