Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wenye matatizo ya akili wajumuishwe katika mipango ya maendeleo

Watu wenye matatizo ya akili wajumuishwe katika mipango ya maendeleo

Shirika afya duniani WHO leo limetoa wito kwa serikali zote duniani, jumuiya za kijamii na mashirika ya misaada kuchukua changamoto ya kuwasaidia mamilioni ya watu wenye matatizo ya afya ya akili na upunguwani katika nchi zinazoendelea.

WHO inasema kundi hilo la watu ndilo lililoko katika hatari kubwa, kwani takribani robo tatu ya mzigo wa watu wenye matatizo ya akili duniani uko katika nchi za kipato cha chini na cha wastani.  Akiyasema hayo katika ripoti mpya iliyotolewa leo iitwayo kuwalenga watu wenye matatizo ya akili kama kundi lililoko katika hatari, mkurugenzi wa WHO Margareth Chan amesema watu hao wameachwa kando hasa katika misaada ya maendeleo na kupewa kipaumbele na serikali.

Ripoti inatoa wito kwa wadau wa maendeleo kutambua matatizo ya kundi hilo na kuwajumuisha katika mipango ya maendeleo , kuongeza huduma za matibabu ya akili, kutoa kwao kama walemavu na kuwahusisha pia katika kuandaa mipango ya maendeleo ya kuwasaidia. Ripoti inasema takribani watu milioni moja wanajiua kila mwaka, ikiwa ni sababu inachochukua namba tatu katika kukatili maisha ya watu hasa vijana.