Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya kimataifa ya demokrasia kauli mbiu ikiwa uwajibikaji wa kisiasa

Leo ni siku ya kimataifa ya demokrasia kauli mbiu ikiwa uwajibikaji wa kisiasa

Leo ni siku ya kimataifa ya demokrasia siku ambayo ilipitishwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1997 baada ya muungano wa wabunge IPU kupitisha azimio la kimataifa la demokrasia.

Siku hii inamaanisha kwamba kusherehekea mafanikio ya demokrasia lakini pia kama kumbusho kwamba haja ya kutetea demokrasia ni muhimu na ni ya haraka sasa kuliko wakati mwingine wowote. Katika ujumbe maalumu wa kuadhimisha siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amehusisha demokrasia na kufikia malengo ya maendeleo ya milenia MDG's na kusisitiza haja ya jukumu muhimu la demokrasia katika kupunguza umasikini na kuchagiza maisha bora kwa watu.

Ban amesema uwazi, uwajibikaji na uongozi bora ni muhimu katika kazi ya kuhakikisha maendeleo yanapatikana. Naye Rais wa IPU Dr Theo-Ben Gurirab akizungumza mjini Geneva katika maadhimisho ya siku hii amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni uwajibikaji wa kisiasa na ni habari njema kuwa nchi nyingi sasa zinaongozwa kwa kufuata mfumo wa kidemokrasia. Rais huyo ambaye pia ni spika wa bunge la Namibia amesema ujumbe wake ni uwajibikaji

(SAUTI YA  DR GURIRAB)