Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nitatumia kila njia kumkomboa mwanamke:Bachelet

Nitatumia kila njia kumkomboa mwanamke:Bachelet

Mkuu wa chombo kipya cha Umoja wa Mataifa chenye jukumu la kupigania usawa wa kijinsia na kumuwezesha mwanamke UN-Women bi Michelle Bachelet Rais wa zamani wa Chile amesema atafanya kila liwezekanalo kusaidia katika ukombozi wa mwanamke.

Akizungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa Bi Bachelet amesema ujuzi alionao na mahusiano na viongozi mbalimbali wa dunia itakuwa moja ya silaha zake katika kufanikisha malengo ya UN Women.

(CLIP MICHELLE BACHELET)

Ameongeza kuwa duniani kote hivi sasa bado kuna baadhi ya nchi wanawake wananyanyaswa, kudharauliwa, kukeketwa, kunyimwa haki zao za binadamu, kukosa elimu kwa sababu tuu wao ni wanawake.

Amesema ana imani kubwa kwa ushirikiano na wadau wengine UN-Women itaweza kuleta mabadiliko katika maisha ya wanawake duniani na hasa wanaotoka katika nchi masikini na kuweza kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.