Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dalili za uvumbuzi zaonekana baada ya msukosuko wa uchumi

Dalili za uvumbuzi zaonekana baada ya msukosuko wa uchumi

Ripoti mpya ya shirika la umoja wa mataifa linalolinda umiliki wa mali WIPO unaonyesha kuwa uvumbuzi zaidi umeanza kushuhudiwa mwaka huu baada ya kuathirika kutokana na hali mbaya ya kiuchumi iliyoikumba dunia kati ya mwaka 2008 na 2009.

Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa wakati dunia ilipoanza kukumbwa na hali mbaya zaidi ya kiuchumi mwaka 2008 mamilioni ya mapendekezo ya kibishara na uvumbuzi mwingine havikutumiwa kote duniani. Katibu wa shirika la WIPO Fancis Gurry anasema kuwa uvumbuzi utakaoshuhudiwa baada ya kulazika kwa hali mbaya ya uchumi utakuwa mkubwa kuliko hata ule ulioshuhudiwa kwa muongo mmoja uliopita .

Hata hivyo ripoti hiyo pia ilionyesha kuwa maombi ya uvumbuzi ya wasio kuwa wenyeweji yaliathirika zadi kuliko ya walio wenyeji. Ripoti hiyo pia imeelezea jinsi wasi wasi wa kichumi ulivyosababisha makampuni mengi kusitisha uvumbuzi wao.