Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watetezi wa haki lazima waungwe mkono:Pillay

Watetezi wa haki lazima waungwe mkono:Pillay

Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ametoa wito wa kimataifa kuwaunga mono watetezi wa haki za binadamu.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa baraza la haki za binadamu mjini Geneva leo, Bi Pillay amelitaka baraza hilo na jumuiya ya kimataifa kuwasaidia watetetezi wa haki za binadamu kwa maneno na vitendo. Amesema watetezi wa haki za binadamu, waandishi habari na wanaharakati wa kijamii wanakabiliwa na vitisho dhidi ya amaisha na usalama wao kwa sababu ya kazi wanazofanya.

Ametaja mashambulizi dhidi ya watetezi hao nchini Iran, Iraq na Somalia, pia vitisho na kunyanyaswa nchini Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Zimbabwe. Pia amesema kuna vikwazo vingi na kunyimwa uhuru dhidi ya watu hao katika nchi za Bahrain, Belarus, Uchina, Misri, Libya, Panama, Syria na Tunisia. Kwingineko kulikotajwa ni mamlaka ya Palestina na Israel, na ambako sheria haitekelezwi ipasavyo dhidi ya amauaji ya watu hao ni Urusi, Azerbaijana, Guetemala, Mexico na Serbia.

(SAUTI YA NAVI PILLAY)

Bi Pillay amesema mara nyini shinikizo dhidi ya watetezi wa haki, vyombo vya habari na jumuiya za kijamii huongezeka wakati wa uchaguzi, akitolea mfano ghasia za karibuni nchini Burundi, Rwanda na Sudan.