Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Malengo ya maendeleo ya milenia ni magumu lakini yanaweza kufikiwa :Ban

Malengo ya maendeleo ya milenia ni magumu lakini yanaweza kufikiwa :Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema malengo ya maendeleo ya milenia MDG ni magumu lakini yanaweza kufikiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York hii leo Ban amesema nchi nyingi masikini zimepiga hatua kubwa na dunia kwa ujumla iko katika mwelekeo wa kupunguza kwa nusu umasikini ifikapo mwaka 2015 jambo ambalo amesema ni hatua kubwa.

Ban amesema anatambua kuwa muda wa mwisho wa kufikia malengo hayo unakaribia na bado kuna nchi ambazo zinajikongoja na pia fedha zinazohitajika bado hazitoshelezi hivyo kuna changamoto.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa utakaojadili hatua zilizopigwa juu ya kufikia malengo ya maendeleo ya milenia unaanza rasmi kesho na utaendelea hadi mwishoni mwa mwezi Novemba. Wakuu wa nchi na serikali 139 wanatarajiwa kuhudhuria.